Tuesday, June 5, 2012

RC Kagera asikitishwa na wakazi wa Kagera kuhama na jina la mkoa huo na vijiji vyake

Mkuu wa mkoa Kagera kanali Fabian Massawe ameonesha kusikitishwa na wanakagera kuhama na jina la mkoa wao pamoja na vijiji na tongoji vyake.
Kanali Massawe ametoa kichekesho hicho leo katika kamati ya Ushauri wa mkoa Kagera unaoendelea sasa hivi katika ukumbi wa ofisi yake mjini Bukoba.
"Kweli aibu na ninasikitika sana ukienda Dar Es Salaam wakazi wa mkoa huu wamehama na jina la mkoa wao hadi kuna sehemu panaitwa magome Kagera, ukielekea  mbezi kuna sehemu panaitwa Nyaishozi... kweli ndiyo sababu hawapendi kurudi kuwekeza kwao"alisema na kjuwaamcha wajumbe wa kikao hicho wakiumia mbavu kwa kicheko.
Alisema kila mkoa kuna hapa nchini kumejaa majina ya maeneo ya Mkoa Kagera, jambo ambalo linampa wakati mugumu, kwani maeneo hayo jinsi yalivyo, yanavutia tofauti na mkoa wao walikozaliwa.

No comments:

Post a Comment