Monday, June 25, 2012

Kuadimika kwa mafuta ya taa, bei yake yapaa kutoka sh. 2280 hadi 3500 kwa lita

Na Theonestina Juma, Bukoba
BEI ya nishati ya mafuta ya taa katika Manispaa ya Bukoba imepanda maradufu kutoka sh. 2280 hadi 3500 kwa lita kutokana na kuadimika kwa nishati hiyo.
Uchunguzi uliofanywa na blog hii katika Manispaa ya Bukoba umebaini wauzaji wa reja reja kwenye maduka  kwa awale walio nayo ndiyo huuwauzia wananchi nishati hiyo lita moja kwa sh.3500.
Bei hiyo imepanda kutokana na nishati hiyo kuadimika katika Manispaa ya Bukoba kwa takribani mwezi moja na wiki mbili sasa ambapo hakuna dalili yoyote inayoonesha kupatikana kwa nishati hiyo.
Katika baadhi ya maduka ya watu binafsi yalioko mjini hapa, ambapo blog hii nayo ilitinga maeneo hayo kwa lengo la kutafuta nishati hiyo, aliishiwa nguvu kuelezwa na wenye maduka hayo kuwa lita moja ni sh. 3500 tofauti na bei inayojulikana kwa wananchi kulingana na bei elekezi ya EWURA.
Kutokana na bei hiyo kuwa juu kuzidi kipimo, baadhi ya wanunuzi ambao walikutwa na blog hii katika maeneo hayo yanayouza nishati hiyo walisikika wakilalamika huku wakiiomba serikali kuingilia kati kuharakisha upatikanaji wa nishati hiyo katika Manispaa ya Bukoba na vitongoji vyake.
Mmoja wa wanunuzi hao aliyejitambulisha kwa jina la mama Shabani alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitaabisha kutafuta nishati hiyo katika vituo vinavyouza mafuta ya taa mjini hapa bila mafanikio ambapo hata wakiwahoji wauzaji  wanashindwa kitu cha kuwaeleza zaidi ya kuwaambia kwua malori yako njiani yanaleta nishati hiyo.
Kulingana na sensa ya mwaka 2002 inaonesha kuwa asilimia 80 ya watu ndiyo wanaishi maeneo ya vijijini ambao ndiyo hutumia zaidi nishati ya mafuta ya taa nyakati za usiku, ambapo kutokan an tatizo hili linaonekana kuwaathiri zaidi wananchi wanaotumia nishati hiyo kwa lengo la kupata mwanga ndani ya nyumba zao.
Hata hivyo kwa baadhi ya wauzaji wa nishati hiyo, akizungumzana blog hii alisema wanamshukuru Mungu kwa kuajalia kufanya biashara katika kipindi hiki, kwani kipindi kirefu  walikuwa hawapati wateja kutokana nwengi walikuwa wakienda kwenye vituo kununua nishati hiyo.

No comments:

Post a Comment