Na Mwandishi Wetu, Bukoba
KIKUNDI cha walemavu wa viongozi
wanaojishughulisha stadi za kazi katika Manispaa ya Bukoba wameiomba serikali kwaongezea
mitaji ili kuweza kununulia malighafi.
Ombi hilo limetolewa leo na baadhi ya
wanakikundi cha walemavu wa viungo wajulikanao kama East African drums Bukoba disabled Assistance Project (BUDAP) wakati
wakizungumza na blog hii katika banda lao la maonesho ya saba saba
yanayofanyika mjini hapa.
Mwenyekiti
wa BUDAP Bw. Issa Zacharia alisema hawapati wateja wa kununua bidhaa zao kutokana
na kukaa nje ya mji na kutokuwa na uwezo wa kupanga chumba kati kati ya mji
jambo ambalo linawaathiri katika biashara zao.
Alisema kikundi
hicho ambacho kinajumla ya wanachama saba wote wakiwa ni walemavu wa viungo,
wanakabiliwa na ukosefu wa kupata fedha
kwa jili ya kununulia mali ghafi.
Halikadhalika
mwanakikundi mwenzake ambaye pia ni mlemavu, Bw. Ashlafu Ramadhani alisema
kutokana na ukosefu wa malighali inawafanya kutengeneza ngoma ndogo ambapo
wakatiwa na malighafi hutengeneza ngoma kubwa ambazo hulazimika kuuza kwa
sh.30,000.
No comments:
Post a Comment