MSANII wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya
mauaji amefikishwa mahakamani leo na kurejeshwa tena mahabusu bila kupandishwa
kizimbani.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akituhumiwa kumuua aliyekuwa muigizaji nyota wa filamu Tanzania, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo April 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kutajwa, lakini hakupandishwa kizimbani na badala yake alirudishwa tena mahabusu katika gereza la Ukonga.

Hata hiyo, taarifa zilieleza kuwa mshtakiwa huyo hakuweza kupandishwa
kizimbani leo licha ya kufikishwa mahakamani kutokana na Mahakama Kuu kuamuru
mwenendo wa kesi hiyo katika mahakama hiyo usimame.
Juni 11 Mahakama Kuu iliagiza mwenendo wa kesi hiyo katika Mahakama ya Kisutu usimame, baada ya kuamua kufanya uchunguzi wa usahihi wa umri wa mshtakiwa huyo, kufuatia maombi ya mawakili wanaomtetea mshtakiwa huyo.
Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata kama ni mtoto au ni mtu mzima, jambo ambalo liliwalazimu mawakili hao kuwasilisha maombi hayo ya uchunguzi wa umri wake Mahakaama Kuu, baada ya Mahakama ya Kisutu kuyaktaa ikisema kuwa haina uwezo wa kisheria kuyashughulikia.
Katika Maombi hayo namba 46 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa Mahakama Kuu Mei 15 na mmoja wa mawakili wake, Peter Kibatala walikuwa wakiiomba Mahakama Kuu itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo.
Walidai kuwa wanaamini Mahakama ya Kisutu ambayo kwa sasa ndio bado inayoshughulikia kesi hiyo, ina mamlaka ya kufanya au kuamuru ufanyike uchunguzi wa umri mshtakiwa huyo.
Hata hivyo waliiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi Mahakama Kuu yenyewe ifanye uchunguzi huo.

No comments:
Post a Comment