Thursday, June 7, 2012

DC mpya wa Bukoba aanza kazi kwa mikwara

IKIWA leo siku ilioteuliwa rasmi kwa ajili ya kufanya usafi kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba, imemlazimu Mkuu mpya wa Halmamashauri ya Bukoba, BI. Ziporah Pangani kuingia mitaani akifuatana na wenyeji wake kuhimiza watu wajitokeze  kufanya usafi katika maaeno yanayowazunguka huku akitumia fursa hiyo kujitangaza kwa watu kuwa ndiye DC mpya wa Bukoba.
Kama hilo halitoshi, huyu mama anaonekana kuwa hana mchezo katika suala nzima ya usafi, kwani leo hii katika maduka yalioko katika barabara ya Uganda amelazimika kuwatoza fani wafanyabishara wawili ambao maeneo yao yalikuwa machafu.
Katika sheria ndogo za Manispaa mtu akikutwa eneo lake chafu kama ni mfanyabiashara hutozwa fani ya sh. 20,000 papo hapokampuni sh. 50,000  na mtu binafsi pia ni sh.10,000/=, ndiyo leo imewakumba wafanyabiashara wawili wa eneo hilo.
Hizo fedha unazitoa hakuna ubishi, na kweli wamezitoa.Katika sakata hili ambalo ni mara ya kwanza kutokea katika Manispaa ya Bukoba, imekuwa gumzo kwa wakazi wa mji huu, huku baadhi yao wakidiriki kusema kuwa  DC wa sasa hana mchezo katika suala la usafi, hivyo kitu kilichobaki ni kuchelewa kufungua maduka.
Wasiopenda usafi, kwani wanapenda kufanyiwa tu, wanadai kuwa watalazimika kuja mjini siku ya alhamisi baada ya ukaguzi wa usafi kupita, lakini si kuja kukabwa ati watu wazima kuinamisha migongo yao kama watoto kufanya usafi! Kazi kweli kweli.

No comments:

Post a Comment