Wednesday, June 27, 2012

Mwili wa mwanafunzi aliyeuwa kikatili wasafirishwa kwenda B'mulo kwa mazishi

Bukoba
 MWILI wa mwanafunzi Advea Makanyaga (16) aliyeuawa kikatili na kisha mwili wake kutupwa shimoni mbugani umesafiriswha leo kwenda wilayani Biharamulo kwa mazishi.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Bishaka, Bw. Rongino ameiambia blog hii leo mchana kuwa mwili huo umesarishwa kwenda wilayani humo baada ya baba yake mzazi Bw. Makanyaga kuwasili juzi mjini hapa kufanya utaratibu wa kusafirisha mwili wa bintiye.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kaagya alikutwa na mauti ya kikatili,baada kupewa chakula na bibi yake mzaa mama yake, Bi. Mareselina Bigira kwa ajili ya kumpeleka mchungaji wao machungani.
Kwa nafasi hiyo huenda ndiyo Bw. Peter Mabara (25) alipata fursa ya kumuua mtoto huyo kutokana na kudaiwa kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa akimtaka kimapenzi lakini alikuwa akimkatalia.
 Bw. Rongino alisema mwanafunzi huyo alikuwa akiishi ujombani ambapo kwa kipindi kirefu ameishi na bibi yake baada ya wazazi wake kutengana. Mwwnafunzi huyo aliuawa kwa kubakwa kwanza na kisha kunyongwa shingo lake na taya la upande wa kulia kuvunja na kishwa mwili wake kutupwa shimoni kwenye korongo, huku kichwa kikiwa chini na miguu juu.

No comments:

Post a Comment