Monday, June 25, 2012

Maporomoko ya Ardhi yauwa watu zaidi ya 100 Uganda


Ramani ya Bududa
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia katika maporomoko ya ardhi Mashariki mwa Uganda. Hii ni kwa mujibu wa maafisa eneo hilo.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Uganda limeambia BBC nyumba 15 zimefunikwa na udongo katika wilaya ya Bududa.
Vijiji vilivyoathirika ni karibu na Mbuga ya Mlima Elgon ambayo hutembelewa na watalii karibu na mpaka na Kenya.
Shirika la Msalaba Mwekundu limetuma kikosi cha wokozi eneo hilo kutathmini uharibifu.
Katibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Uganda Michael Richard Nataka ameambia BBC kwamba katika kijiji komoja nyumba 15 zimefunikwa huku watu wengi wakikwama kwenye makazi yao huko Bududa.
Tayari watu 20 wamethibitishwa kufa na idadi hii huenda ikaongezeka.
Awali maafisa walisema watu kati ya 20 hadi 100 waliangamia. Eneo hilo limeshuhudia mvua kubwa katika siku za karibuni.
Hapo Agosti mwaka jana watu 24 walikufa baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi katika Wilaya ya Bulambuli Mashariki mwa Uganda. Mwaka 2010 watu 100 walikufa katika Wilaya Bududa baada ya maporomoko ya arthi.

No comments:

Post a Comment