Thursday, May 31, 2012

Zuku kudhamini tamasha la kimataifa la Zanzibar

Mwenyekiti wa kampuni ya  Wananchi Group kampuni inayosambaza vin'gamuzi vya televisheni ya Zuku Afrika hapa nchini Bw. Ali Mufuruki akizungumza katika hafla ya kutangaza kampuni hiyo ya Zuku Kudhamini tamasha la kimataifa la  Zanzibar International Film Festivala (ZIFF) katika hafla iliyofanyika jana kwenye ufukwe wa Slipway jijini Dar  es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tamasha la ZIFF wakiwemo wanamuziki, waigizaji wadhamini na wengeni wengi.
 Mmoja wa wasanii wa kundi la Shilole akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo jana jioni.
 Waigizaji wa filamu mbalimbali wakiwa wamesimama mbele wakati walipokuwa wakitambulishwa katika hafla hiyo na mwenyekiti wa ZIFF Bw. Mahmoud Thabit Kombo.
 Kutoka kulia ni Jacob Steven. Raymond Kigosi na Cloud waigizaji wa filamu za Bongomovie wakiwa katika hafla hiyo..
 Mchekeshaji Steve Nyerere kulia akiwa na wadau kutoka kampuni ya kusambaza filamu ya Steps Entertainment.
 Mwigizaji Jaquiline Walper kushoto akiwa na waigizaji wengine katika hafla hiyo wa tatu kutoka kulia ni mchezaji wa timu ya Simba Uhuru Selemani.
 Mwigizaji Aunt Ezekiel kushoto akiwa na waigizaji wenzake.
 Mwanamuziki Shilole akitumbuiza na kundi lake katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa ZIFF Bw. Mahmoud Thabit Kombo akiwatambulisha waigizaji pamoja na wasanii mbalimbali katika hafla hiyo jana.

No comments:

Post a Comment