Kwa hisani ya www.mamapipiro.blogspot.com
TIMU ya taifa ya wanawake ya
Tanzania, Twiga Stars, imeanza vibaya kampeni za kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Kombe la Mataifa kwa wanawake, baada ya kufungwa mabao 2-1
jana jioni mjini Addis Ababa na wenyeji, Ethiopia.
Twiga sasa inahitaji ushindi wa
1-0, Juni 16, katika mchezo wa marudiano mjini Dar es Salaam, ili kukata tiketi
ya kucheza fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo, Novemba mwaka huu,
Equatorial Guinea, zikiwa ni za nane katika historia ya michuano
hiyo.
No comments:
Post a Comment