Friday, May 25, 2012

Utawezaje kumtambua mchawi? hapa mjadala wa uchawi ukiwa umepamba moto

 Bw. Mayunga Kidoyayi Mwangalizi wa haki za Binadamu Wilaya ya Bariadi ambaye pia ni Katibu wa mila na desturi mkoa wa Shinyanga akijadili kuhusuMchawi na Mganga  ambapo hapa alilazimika kutumia hisia kali kuelezea uganga nini na mchawi ni nani.
 Mjadala wa uchawi ukiwa umepamba moto, hata Mchungaji wa kanisa la Neema  Kuu, Devis Shyogetera wilayani Ngara naye akitoa mchango wake juu ya uchawi ambao alisema kuwa ni wakala wa shetani., na kwamba ni wabaya sana kutokana na kutesa watu, hivyo sheria ibadilishwe ikithibitika kuwa ni mchawi ahukumiwe miaka hata 30 au kifo.Biblia inasema usimwache mwanamke mchawi aishi.
 Bi. Jacquilene Justine Bahebe aliyesimama akitoa ushuhuda namna shangazi yake alivyomwamuru kukoroga uji katika masufuria makubwa bila kujua kuwa kumbe alikuwa akiwakorogea msukule waliochukuliwa na shangazi yake aliokuwa akiwafuga ndani ya nyumba yake.Shangazi yake huyo ambaye hakumtaja jina lake alijinyonga siku hiyo hiyo usiku wa manane kukwepa aibu ya wananchi baada ya binti huyo kitibua.
Pichani wa kwanza kushotom ni Vick Maro wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga ambaye yuko katika dawati la kutetea haki za binadamu ambapo awali alifanya kazi hizo akiwa katika kituo cha kivulini Jiji Mwanza kabla ya kujiunga na jeshi hilio, wa pili ni mwanagalizi kutoka Dodoma mjini, Bw. Maclean Mwamlangala ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu chaSt. John mkoani Dodoma, anayemfuata ni Bi . Angela Benedicto  ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa ndani kutoka jijini Mwanza na pia ni mwangalizi wa Wilaya ya Nyamagana jijini humo.

No comments:

Post a Comment