Monday, May 14, 2012

Siku ya familia duniani karibu tusemezane

KESHO ( Mei 15 kila mwaka) ni siku ya Familia Duniani, Watanzania wote tunaungana na dunia nzima kuadhimisha siku hii.Lakini wakati tunaadhimisha siku hii, ikumbukwe kuwa bado Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya siku ya siku ya familia duniani kutokana na kuwepo kwa vitendo vingi  vya unyanyasaji wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia.

Watoto wanafanyiwa ukatili wa kutisha ndani ya familia.Mfano kama katika Manispaa ya Bukoba takribani wiki tatu zilizopita watoto wawili wa kike wenye umri wa miaka minne walirubuniwa na watu wanaoishi nao katika familia moja na kuwabaka na kuwaharibu vibaya sehemu zao za siri  hadi kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa wiki nzima.

Watoto hawa mmoja anaishi mtaa wa Kashabo kata ya Hamugembe na Mwingine ni mtaa wa Nyakanyasi kata ya Bakoba, mitaa yote haya yanapakana tu, na inasemekana kuwa wabakaji hao wakati wakiwafanyiwa watoto hawa vitendo hivyo, huwafunika macho na midomo yao kwa kutumia kitambaa cheusi.

Inasikitisha watu hawa wanafanya vitendo hivi, Jeshi lipo, watoto wanalazwa hospitalini hadi wanruhusiwa, Jeshi halijapata taarifa, hadi wapelekewe taarifa na Waandishi wa habari, ndipo wanashtuka, wakati katika Jeshi hilo, kuna dawati linaloshughulikia masuala ya jinsia, hasa za unyanyasaji na upuuzi kama huu, hakuna hatua madhubuti za kuchukua, kweli hakuna haja ya kuadhimisha siku ya familia.

Huu ni ukatili wa kutisha, ni unyanyasaji uliopitiliza, unyanyasaji na ukatili unaofanyiwa viumbe visivyokuwa na uwezo hata wa kujitetea.Ukatili unaotakiwa kupingwa kuanzia ngazi ya familia hadi taifani.Ukatili usiotakiwa kufumbiwa macho.

No comments:

Post a Comment