Na Mwandishi wetu
MREMBO anayeshikilia
taji la Miss Universe Tanzania 2011/2012 Nelly Kamwelu kwa kushirikiana na Mfuko
wa Saratani ya Matiti Tanzania (Breast Cancer Foundation) leo atafanya harambee
ya kuchangia mfuko wa saratani ya matiti itakayofanyika kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Harambee hiyo imepangwa
kuanza saa 1.00 usiku kwa mujibu wa muandaaji wa mashindano ya Miss Universe
Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Commutations, Maria
Sarungi.
Maria alisema kuwa
katika hafla hiyo kutakuwa na mnada wa kito cha Tanzanite ambayo imetolewa
maalum na kampuni ya Richland Resources kwa ajili ya kuchangia
mfuko huu. Pia picha ya Mrembo wa Miss Universe Tanzania itanadiwa katika mnada
huo.
Mrembo Nelly Kamwelu
toka achukue taji la Miss Universe Tanzania 2011, amekuwa akifanya kazi bega kwa
bega na mfuko wa saratani ya matiti ikiwamo kusaidia kutoa elimu katika shule
mbalimbali ili kupunguza au kutokomeza uwezekano wa kuenea kwa saratani ya
matiti. Mfuko huu umepanga kuendeleza elimu hii kwa shule za mikoa ya Mbeya,
Ruvuma, Rukwa, Iringa, Mtwara na Lindi.
Kwa kusindikiza hafla hii kutakuwa na maonyesho ya
mavazi yaliyotolewa na wabunifu wa hapahapa nchini ambao ni Escado Bird, Kemi
Kalikawe na Subira Wahure vilevile kutakuwa na burudani ya muziki kutoka msanii
Enika na mchekeshaji Evans Bukuku. Pia mrembo mwenyewe Nelly Kamwelu atatoa
burudani ya dansi aina ya Belly Dance.
No comments:
Post a Comment