HATIMAYE
kitendawili cha lini atazikwa rasmi Kadinali wa kwanza wa Mwafrika, Laurian
Rugambwa aliyefariki dunia takribani miaka 14 iliopita imeteguliwa baada ya
kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba kutangaza siku ya kuhamishwa mwili wake kutoka katika kanisa Katoliki Parokia ya Kashozi
alikozikwa kwa muda na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Kwa mujibu
wa tangazo lililochapwa katika gazeti linalomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo
la Bukoba linalojulikana kwa jina la RUMULI toleo namba 268 ya mwezi Aprili
mwaka huu, mwili wa Muadhama Kadinali Rugambwa unatarajiwa kuhamishwa rasmi
Oktoba 6, mwaka huu kutoka Kanisa la Kashozi na kuzikwa ndani ya Kanisa kuu la
Jimbo hilo lililochukua takribani miaka 12 kukamilika kwa ukarabati wake.
Kwa mujibu
wa tangazo hilo, ibada maalum ya kuhamisha mwili na kuuzika itafanyika katika
kanisa hilo kuu la Bukoba siku hiyo ya Oktoba 6, mwaka huu majira ya saa 9
alasiri.
Aidha
Oktoba 7, mwaka huu imeelezwa katika tangazo hilo kuwa itakuwa ni siku ya kubarikiwa kwa
kanisa hilo na kumbukumbu ya miaka 100
ya kuzaliwa kwa kadinali huyo wa kwanza Mwafrika.Kadinali Rugambwa alifariki dunia mwaka 1997.
mwisho.
No comments:
Post a Comment