Wanafunzi wa shule ya msingi Kising'a
Isimani wilaya ya Iringa vijijini wakiwa wamebeba ndoo za maji kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba ya mwalimu jana majira ya saa 9.45 asubuhi muda ambao
walipaswa kuwepo darasani kama walivyokutwa na mpiga picha wetu (picha zote
na Blog ya Francis Godwin)
Na Blog ya Francis Godwin
TABIA
ya uongozi wa shule ya msingi Kising'a Isimani wilaya ya Iringa
kuwatumikisha kazi wanafunzi asubuhi wakati wa vipindi vya masomo imepingwa
vikali na baadhi ya wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule hiyo na
kuiomba wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuingilia kati suala
hilo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi leo kijijini hapo
wazazi hao walisema kuwa uongozi wa shule hiyo ya msingi Kising'a kila
siku kabla ya watoto kuingia madarasani wamekuwa wakiwatuma katika kazi
mbali mbali ikiwemo ya kuchota maji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya
mwalimu.
Alisema Jonh Kalinga kuwa tayari wamepata kuulalamikia
uongozi wa shule hiyo na kuukanya kacha kuwatumikisha watoto hao majira
ya masomo ila bado vitendo hivyo vya wanafunzi kukatishwa vipindi na
kwenda kufanya kazi za walimu vimekuwa vikiendelea.
|
No comments:
Post a Comment