BAADA ya vurugu na maandamano na
kuchomwa moto baadhi ya makanisa zilizosababishwa na Kikundi cha Uamsho,Serikali
imetakiwa kuunda tume ya kukichunguza kikundi hicho chenye mwuelekeo kama
Al-Shabab cha nchini Somalia.
Kauli hiyo
ilitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislam (TIPF), Sadiq Godigodi,
wakishirikiana na mwanaharakati Chifu Msopa jijini Dar es Salaam jana kuwa
wanalaani vugurugu zote zilizosababishwa na kikundi hicho.
"Watanzania
tunapaswa kuwa makini na Kikundi hiki kwani sisi tukiwa Waislam tunaifahamu
vizuri historia ya Al-Shabab ilivyoaanza kwani walianza kama hivi sasa hatutaki
kuingiza nchi hii katika matatizo ya kuuwana kama ilivyotokea nchini Rwanda
1994"alisema Godigodi.
Alisema
wanaitaka serikali kukichunguza kikundi hicho kwa kuwa kinakwenda kinyume na
malengo yake, kwani kilianzishwa kwa ajili ya kufanya mihadhara, kueleimisha,
maadili ya dini, kufanya ibada na mambo yote anayohitaji Mungu (Alla SW).
Aidha,
wanalaani vurugu zote zilizosababishwa na baadhi ya watu wa Uamsho kwa kusema
makanisa hayakutendewa haki hata kidogo kwa kuwa kanisa si serikali wala Tume ya
Uchaguzi au Chama cha siasa.
Godigodi
alikwenda mbali kwa kusema wanawalani wale wote wanaopinga muungano kwani hata
Mwenyezi Mungu anawachukia wote wanaotaka kujitenga au kufanya ubaguzi wa aina
yeyote ya Dini, Kabila au rangi, kwani Mwenyezi Mungu aliwawakea misingi ya
kuheshimu dini za watu wengine na wale wasiokuwa na dini.
Godigod alisema
Waislama wanakishangaa kikundi hicho kwa kufanya mihadhara ya kuleta chuki kwa
baadhi ya Waislama wa Zanzibar kama vile kupinga muungano wa Zanzibar na
Tanganyika wakati kuna utaratibu umewekwa wa kutoa maoni kuhusu suala
hilo.
Vile vile
kuwakataa baadhi ya watu kutoka Bara wanaoishi kuondoka Visiwani humo kama
walivyosoma katika vyombo vya habari (huu ni ubaguzi), na kupinga utoaji wa
maoni kuhusu mchakato wa Katiba mpya.
Hata hivyo,
alisema Zanzibar ni Kisiwa chenye idadi kubwa ya waislam na vyama vikubwa vyenye
idadi kubwa ya wanachama ambapo vyama hivyo vina ushawishi kwa wananchi
mbalimbali.
Alisema baada
ya muafaka wa CCM na CUF Wazanzibar wamekuwa kitu kimoja wakishirikiana kwa kila
jambo ni dhahiri kwamba kila Mzanzibari anhitaji maisha ya umoja na
ushirikiano.
Hata hivyo kuna
taarifa kuwa Serikali ya Mapinzi Zanzibar imesimamisha shughuli zote za Kikundi
hicho cha Uamsho.
No comments:
Post a Comment