Mwanza
Ni jambo la kusitikisha na kuhuzunisha kwa mwananchi wa kawaida akisikia kuwa hata hospitali ya Rufaa ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza, wagonjwa wanalazwa wawili wawili katika kitanda kimoja.
Kwa mwananchi wa kawaida hasa yule anayeishi kijijini, akizipata taarifa hizi hawezi kuziamini, kulingana na ukongwe wa hospitali hii na umaarufu wake katika ukanda wa Ziwa.
Kweli, naomba huyo mkulima wa kijijini, aamini hivyo, kuwa katika hospitali ya Rufaa ya Bungando katika baadhi ya wodi wagonjwa wanalala wawili wawili katika kitanda kimoja.
Hapa mkulima wangu huyo, au hata mtu wa kawaida ambaye hajafika hospitalini hapo, labda huenda anafika lakini hajabahatika kufika katika baadhi ya wodi hizo, basi afike katika wodi namba 5J chumba namba 2 atakumbana na hali hiyo.
Lo, kweli inasikitisha kwani wodi hii ni ya wanawake wanaoumwa hasa sehemu za miguu, yaani wale waliovunjika miguu au mikono, huwezi aamini wanalala wawili wawili.
Lakini katika utafiti wangu wa haraka haraka bila kibali ya utafiti huo, umebaini kuwepo wodi namba 5J kuwa na vitanda vilivyo wazi, lakini cha kushangaza hakuna hata dalili za kuwatenganisha hao wagonjwa wanolala wawili kitanda kimoja, kwenda katika vyumba hivyo, mfano chumba namba 3 na 4. Labda watafanya mabadiliko hayo leo usiku au kesho.
Hawa ni baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza wakiwa wanalala wawili wawili katika kitanda kimoja.Hata hivyo, wanaangalia ni namna gani mgonjwa huyo alivyovunjika mguu na aina ya mgonjwa kama ni mzee.
Hawa wagonjwa wanalala kitanda kimoja.
No comments:
Post a Comment