Monday, May 28, 2012

Simba yawaacha nyota wake akiwemo Kango

Taarifa zilizothibitishwa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema uongozi wa timu hiyo umewatupia vilago nje wachezaji wake Derrick Walulya kutoka nchini Uganda na Gervas Kago kutoka Jamhuri ya Kati ambao waliitumikia klabu hiyo msimu wa ligi  uliomalizika.
Hatua hiyo pengine imekuja baada ya wachezaji hao kuchezea benchi karibu msimu mzima wa ligi wakiwa nje ya uwanja ukiacha Gervas Kago ambaye angalau kwa michezo kadhaa ya Ligi kuu ya Vodacom alikuwa akiingia dakika chache kabla ya kuisha kwa mchezo.
Hii inaonyesha kuwa Simba  watasajili wachezaji wengine ili kuziba mapengo ya wachezaji hao ambao wamewaacha.

No comments:

Post a Comment