Friday, May 18, 2012

Kuingia Hospitali ya Bugando sasa sharti uvae kiheshima

KAMA ni kuonesha kizazi cha sasa kinakoelekea siko kulingana na mavazi yao, uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza umepiga marufuku uvaaji wasiozingatia staha.
Kwa mujibu wa tangazo lililobandikwa katika mbao la matangazo wa hospitali hiyo, haruhusiwi mtu yeyote aliyevaa mavazi yasiostahili kuingia hospitalini humo, haliishi unakwenda kumwona mgonjwa ama la.
Mavazi ambayo hayatakiwi ni pamoja na mlegezo kwa wanaume wanaovaa masuruali chini ya viuno vyao, kwa wanawake hawatakiwi kuvaa nguo zinazobana.
Wananchi wanapaswa kuvaa nguo za staha na si za kuaibisha, kulingana na tangazo hilo ambalo halina tarehe, wala mwaka.
Sasa wale wanaoingia kwenye nguo za kubana, milegezo, miwani meusi tiii... ni.muda wenu sasa mjifunze kuvaa nguo za heshima bila hilo, sijui mtapitia wapi.
Kwani hata katika dodosa langu katika hospitali hiyo waliokuwa wakiingia hospitalini hapo, awe mgonjwa ama anaenda kuwatembelea wagonjwa wote walikuwa katika mavazi rasmi na za heshima.
 Hata hivyo ushauri wa bure kwa wanawake nadhani kwao hawana taabu kwani waingie kwenye vazi la kangha, nadhani hili ni vazi nadhifu sana hata kama kwa ndani umetinga mini kwa wale ambao wakivaa mavazi marefu mapaja yao yanawawasha.
Kazi kwenu.

No comments:

Post a Comment