Twiga
Stars inacheza leo (Mei 27 mwaka huu) na Ethiopia katika mechi ya
kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC)
kuwania tiketi ya kucheza fainali zitakazofanyika Novemba mwaka huu
nchini Equatorial Guinea.
Mechi
hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa saa za nyumbani itafanyika kwenye
Uwanja wa Taifa ulioko jijini Addis Ababa na timu hizo zitarudiana Juni
16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka Addis Ababa, wachezaji wa Twiga Stars ambayo
imefikia hoteli ya Churchil, leo saa 4 asubuhi wamefanya mkutano wa
mwisho wa maandalizi ya mechi hiyo na kocha wao Charles Boniface Mkwasa
na baadaye kupata chakula cha mchana kwa Balozi wa Tanzania nchini
Ethiopia.
Twiga Stars;
Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Evelyn
Sekikubo, Mwapewa Mtumwa, Etoe Mlenzi, Mwanahamisi Omari, Ester
Chabruma, Fatuma Mustafa na Asha Rashid.
Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said, Semeni Abeid, Zena Khamis, Amina Ally, Rukia Hamis na Fadhila Hamad.
Mchezo
huo unachezeshwa na Angelique Tuyishime akisaidiwa na Sandrine
Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga wote kutoka Rwanda.
Kamishna ni Catherine Adipo kutoka Uganda.
No comments:
Post a Comment