WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametua Visiwani Zanzibar leo ambapo amekemea vitendo vya vurugu,akiahidi Serikali kuwachukulia hatua ikibidi hata kuwavizia nje ya misikitikwa wale watakaohusika na uvunjifu wa amani .
Waziri Nchi aliwasili Mjini Zanzibar akiwa na Mkuu wa
Jeshi la Polisi,Inspekta Jenerali Said Mwema kwa pamoja waliitisha mkutano
uliowakutanisha viongozi wa Jumuiya ya Maimamu
Zanzibar(JUMAZA),Mabalozi, Kamisheni ya Utalii, Jumuiya ya Uamsho na
Mihadhara ya Kiislam Zanzibar(JUMIKI).
“Suala la kufuata sheria halina mjadala,lazima kila
mmoja wetu afuate na kutii sheria hatutawavumilia watakaovuruga amani ya
nchi…maandamano yoyote lazima yapate kibali” Aliwaambia wadau katika mkutano huo
uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar,Ziwani.
Waziri Nchi alisema busara ya Polisi imefikia kikomo na
kwamba atashangaa sana akiona busara hiyo ikiendelea wakati kuna watu au kikundi
kinavunja amani ya nchi.
“Tutashangaa busara ya Polisi ikiendelea wakati watu
wanaumia kwa watu wengine kuvunja amani…hatutakubali, tutaendelea kuviziana hata
nje ya misikiti tutawakamata” Alisisitiza Waziri Nchi.
Waziri huyo alisema kila mtu anawajibika kitunza amani
iliyopo ambapo pia alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja
wa Kitaifa imefanyakazi nzuri katika kipindi kifupi na kuwapongeza Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa
Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif
Ali Idd.
MWISHO
No comments:
Post a Comment