Thursday, May 10, 2012

Utaratibu huu wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando ni wa kuigwa

Ni kipindi kirefu sijawahi kufika katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuwajulia wagonjwa hali zao.Pamoja na kwamba ni kipindi kirefu, si kwa ajili ya matakwa yangu,la hasha, bali ni kutokana na kuwa mbali na Jiji la Rock City.
Lakini nilipoenda hospitalini hapo kwa kweli nimefurhishwa na utaratibu wa hospitali hiyo kutoa uji na chakula cha mchana kwa wagonjwa.
Utaratibu huu ni la faraja sana kwa upande wa baadhi ya wagonjwa wasio kuwa na ndugu wa uhakika wa kuwapelekea chakula hasa kwa wale watoka mbali.
Kwa stahili hii, inawafanya waonekane wako sawa ndani ya wodi walimolazwa wagonjwa wa aina mbali mbali wanaotoka katika familia tofauti wenye uwezo na wasio na uwezo achilia mbali mbali vyakula wanaopelekewa jioni saa 10.
Hata hivyo, hakuna mtu anayependa kuumwa hadi kufikia hatua ya kulazwa hospitalini, wala hakuna anayependa ndugu yake aumwe hadi kulazwa katika hospitali hiyo.
Lakini kwa utaratibu wa wagonjwa kupewa chakula cha mchana hospitalini hapo, kwa namna moja ama nyingine umeweza kusaidia wale wanaowapelekea chakula wagonjwa kuendelea kufanya shughuli zingine za kuwapatia riziki, kama kwa wale wanaokwenda kazini. Ambao hawapati muda wa kuwaandalia chakula  stahiki kwa wagonjwa wao. 
Heko kwa uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Bugando.

No comments:

Post a Comment