Thursday, May 31, 2012

UKatili wa kuwalawiti watoto washamiri kwa kasi Karagwe-DC

                         Na Mwandishi Wetu, Karagwe
BAADA ya vitendo vya ubakaji kupungua kwa watoto wa kike na wanawake wilayani Karagwe, Mkoani Kagera inadaiwa kuibuka kwa vitendo vya ulawiti kwa watoto wadogo, imeelezwa. 
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo, Kanali Mstaafu Issa Njiku ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Misenyi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Wilayani humo.

Kanali Njiku alisema kuwa baada ya vitendo vya ubakaji kupungua kwa watoto walio dhini ya umri  na kukithiri kuwa sasa kumezuka vitendo vya ulawiti kwa watoto wadogo katika wilaya hiyo na kuripotiwa ofisini kwake.

Alisema kuwa vitendo hivi vya aibu ni ukikukaji wa haki za binadamu, kuwa anasikitika kuona kuwa wazazi wengine wanahusika kuwalawiti  hata watoto wao wakuzaa.

“ Mzee mwenye umri wa miaka 54 ameletwa ofisini kwangu hapa Karagwe kwa kosa la kumlawiti mtoto mdogo wa miaka 10, polisi wakikamilisha kazi yao tutampeleka mahakamani huu  si unyama kweli” Alisema Njiku.

Alisema kuwa vitendo hivi vinavyosababishwa wa baadhi ya vijana wanaokunywa madawa  ya kulevya ni pamoja na unywaji wa vinywaji vikali ikiwemo uvutaji wa bangi ambao alisema  hata katika wilaya hiyo umekithiri.

Aidha aliongeza kuwa mkakati uliotumiwa na kamati ya ulinzi usalama katika wilaya hiyo kwa kuhakikisha vitendo vya ubakaji na mimba za utotoni zina pungua hata vitendo hivi vichafu vitakomeshwa  ambapo pia kuwa watawashirikisha wananchi wema kuwafichua watu hao wabaya.

Hata hivyo amewataka wazazi katika wilaya hiyo kuka a karibu na watoto wao kwa muda wote  na kuwasaidia katika malezi mamea na kuacha tabia ya kuwatuma kwenye  vilabu vya pombe na majira ya usiku.

No comments:

Post a Comment