Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera (KRFA) na MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Amir
Roshan, amefariki dunia na kuzikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini
Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ni kwamba shirikisho hilo limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Roshan ambaye alikuwa akiwakilisha mikoa ya Kagera na Shinyanga na kwamba alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu tangu afanyiwe operesheni ya kichwa mwishoni mwa mwaka 2010.
Wambura alisema Roshan alianza kuingia kwenye uongozi wa TFF (wakati huo FAT) katika uchaguzi uliofanyika mjini Kibaha mwaka 1993 na aliendelea kuwa kwenye soka hadi mauti yalipomkuta.
Alifafanua kuwa kiongozi huyo alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwa vipindi vitano mfululizo, alianza kuchaguliwa katika uchaguzi wa mwaka 1993 uliofanyika Kibaha na baadaye akachaguliwa katika uchaguzi wa mwaka 1996 jijini Dar es Salaam, kisha jijini Arusha mwaka 2001, na Dar es Salaam miaka ya 2004 na 2008.
“Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, ameelezea masikitiko yake na mshtuko mkubwa kutokana na kifo cha kiongozi huyo wa muda mrefu kwenye mpira wa miguu nchini, hasa Kanda ya Ziwa, akiwa Mwenyekiti KRFA,” alisema Wambura katika taarifa yake.
chanzo ni Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment