Saturday, May 19, 2012

Chelse waibuka mabingwa wa wapya UEFA

TIMU ya Chelse imeibuka mabingwa wapya wa ligi ya UEFA baada ya kuifunga timu ya Bayern Munich kwa jumla ya penalt 4 -3, baada ya timu hizo kucheza dakika 120 wakiwa wamefungana mabao 1-1.
Aliyeifanya Chelse kuibuka mabingwa wa UEFA ni DIDIER Drogba ambaye aliweza kusawazisha bao dakika ya 88 katika kipindi cha kwanza mpira uliotokana na kona, ambapo Bayern Munich wao walipata bao la kuongoza mnamo dakika ya 83 kupitia mchezaji wao  Thomas Muller mpira uliotokana na mpira wa adhabu.
Hata hivyo,katika muda wa nyongeza wa dakika 30, Drogba alimwangusha mchezaji wa Bayern aliyekuwa amevaa jezi namba 7 katika eneo la Hatari, ambapo mwamuzi aliamua ipigwe penalt  ambayo ilipigwa na Robben na kupanguliwa na kipa Czec wa Chelse.

No comments:

Post a Comment