Na Mwandishi Wetu
BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma
inatarajia kuwapa burudani kabambe wakazi wa Kitunda na maeneo jirani kwa
kufanya onyesho kwenye ukumbi mpya wa Msige Pub Juni 10, mwaka huu.
Mratibu wa onyesho hilo, George Msige, alisema kuwa maandalizi yamekamilika na amewataka wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi kupata vionjo vya wakongwe hao.
Alisema amevutiwa kuialika bendi hiyo kutumbuiza kwenye ukumbi huo uliopo Kitunda Kibeberu, kutokana na maombi aliyopewa na mashabiki wengi baada ya kufurahishwa na 'shoo' ya kwanza ya kundi la taarab la Five Stars wiki mbili zilizopita.
"Kwa hiyo wakazi wa Kitunda Kibeberu kuanzia sasa watakuwa wanapata burudani ya kila aina kwa nia ya kukata kiu yao hivyo, wajiandae kucheza nyimbo za bendi ya Msondo," alisema Msige.
Alisema kuwa Msondo itapiga vibao vya zamani na vipya ambavyo ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga.
Mwimbaji nguli Maalim Gulumo 'Kamanda' na Saidi Mabela na wengineo watafanya vitu vyao siku hiyo ili kukonga nyoyo za mashabiki wao.
Msemaji wa bendi hiyo, Rajab Mhamila 'Super D' amethibitisha Msondo itaangusha burudani ya nguvu katika ukumbi huo ikitokea Masasi, Mtwara kuzindua ukumbi wa Emirate.

No comments:
Post a Comment