Thursday, May 31, 2012

Wabunge wa CHADEMA walivyoagwa rasmi nchini Brazil

Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter  Msigwa na  Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011  waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.
Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo  Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa.
Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani. 
Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo  Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Forward wa United States Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku alidhibitiwa na Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki.
Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la  kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar
Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment