Mbeki Mbeki, Karagwe
MVUA zinazoendelea kunyesha katika Wilaya ya Karagwe
Mkoani Kagera imeleta madhara makubwa ya kuharibu miundombinu ya barabara,
ikiwemo mazao ya kilimo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari Diwani wa Kata ya
Kihanga Josephat Kibate alisema kuwa barabara kuu kutoka mjini Kayanga kuelekea
Bukoba mjini imefungwa kwa muda kutokana na kukatika kwa daraja na mafuriko
makubwa yaliyopelekea barabara hiyo kuharibika kabisa.
Bw. Kibate alisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha tangu
Aprili 30, mwaka huu hadi hivi sasa zimeleta maadhara makubwa ya kuharibu miundo mbinu ya
barabara pamoja na mazao yalioko mashambani.
Alisema mvua hizo zimekata mawasiliano kati ya Kata na
Kata na Wilaya na Wilaya na kamba kwa muda wa siku tatu magari yote
ya abiria hayakuweza kusafiri na wananchi walishindwa kufanya shughuli zao za
maendeleo.
Aliongeza kuwa zaidi ya hekari 50 za maharage katika Kata
yake zimeharibiwa na mvua ni pamoja na na kahawa ambayo kwa kipindi hiki alisema
mvua zinapoendelea kunyesha zao hilo uharibika na kuharibu uchumi wa Wilaya na
Taifa.
Kwa upande wake, Diwani kwa Kata ya Kibondo Jean Adamu
alisema kuwa barabara inayotoka Katani kwake yenye urefu wa km 30 kuelekea Makao
makuu ya Wilaya imeharibika sana ambapo aliongeza kuwa magari makubwa ya
wafanya biashara yamekwama katika barabara hiyo kutokana na mafuriko.
Alisema kuwa barabara hiyo imekuwa korofi kwa muda mrefu
kutokana na kujengwa chini ya kiwango, na kuwa nyakati za mvua abiria wamekuwa
wakipata usumbufu kutokana na maji mengi kutuama barabarani.
Aidha kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Mstaafu Issa Njiku
akizungumzi suala hilo kwa njia ya simu kutoka Dodoma alikiri kuwepo kwa
hali hii ya mafuriko katika sehemu mbalimbali za Wilaya yake na wananchi wengi
kuathirika kutokana na mafuriko hayo.
Hata hivyo amewataka wananchi Wilayani humo wanaoishi
katika mabonde kuhama mara moja katika maeneo hayo kuwa hategemei kusikia lawama
baadae zikielekezwa kwa Serikali kutokana na Ofisi yake kutoagiza hilo kwa wananchi.
“ Nimekuwa mara kwa mara nawaagiza wananchi kuepuka kujenga
mabondeni lakini baadhi ya wananchi ni wagumu kutekeleza maagizo hayo madhara
yake wameathiriwa na mafuriko” Alisema Njiku.
No comments:
Post a Comment