Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na
kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya
vurugu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu
Zanzibar jana,Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote,atakayethubutu
kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”
Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo
vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya
Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha
hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa
stamp ya uvumilivu wa kidini.
“Kwa masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo
vilivyotokea vya kuvunja amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya
wananchi lazima wajue kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile”
Alisema Rais Dk. Shein.
No comments:
Post a Comment