Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya mjini The Hague,
leo inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya aliyekuwa rais wa Liberia Charles
Taylor.
Baada ya kesi iliyodumu miaka sita, Taylor alipatikana na makosa kumi na moja
ya kufadhili na kusaidia waasi nchini Sierra Leone, ili apate madini ya
almasi.Bwana Taylor ni kiongozi wa kwanza wa zamani kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa tangu kumalizika kwa vita vya pili.
hukumu ndefu
Anatarajiwa kupewa adhabu kali ambayo atatumikia katika gereza nchini Uingereza.Upande wa mashtaka unapendekeza Bw Taylor apewe kifungo cha miaka 80 jela. Hata hivyo, upande wa utetezi unadai hukumu hiyo itakuwa kali mno.
Taylor, mwenye umri wa miaka 64, anasisitiza hakutenda kosa lolote na huenda akakata rufaa hukumu itakapotolewa.
Iwapo atakata rufaa, kesi hiyo huenda ikaendelea kwa kipindi cha miezi sita.
ajitetea
Katika uamuzi uliotolewa mwezi Aprili, mahakama maalum inayosikiliza kesi ya Seirra Leone, ilimpata Taylor na makosa kumi na moja, yakiwemo ya ubakaji na mauaji.Katika kujitetea, Taylor alishutumu upande wa mashitaka kuwalipa na kuwatisha mashahidi katika kesi hiyo.
Pia aliwaambia majaji katika kesi hiyo wazingatie umri na afya yake wanapotoa hukumu dhidi yake, akisema'' yeye sio tisho kwa jamii''.
No comments:
Post a Comment