WAZIRI
wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge) Wiliam Lukuvi awa mbunge
wa kwanza wa chama cha mapinduzi (CCM) kukubali kuwekwa kitimoto na wapiga kura
wake katika mwendelezo wa midahalo ya wabunge na wapiga kura wao.
Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani amekubali kuwekwa kitimoto katika mdahalo huo uliopangwa kufanyika Juni 2 siku ya jumamosi katika ukumbi wa Hima kata ya Isimani majira ya asubuhi .
Hatua ya Lukuvi kukubali kuwekwa kitimoto imekuja huku zikiwa zimepita siku chache toka mbunge wa jimbo la Kilolo kupitia CCM Prof. Peter Msolla kukwepa kushiriki mdahalo kama huo uliofanyika katika ukumbi wa Upendo Ruaha Mbuyuni wiki iliyopita .
Mbunge Prof Msolla ambaye amepata kuwa waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia alikwepa mdahalo ulioandaliwa na azaki za kiraia mkoani Iringa chini ya uratibu wa asasi ya ISICO .
Mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa midahalo hiyo ambayo ilianza kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) imepangwa kufanyika majimbo manne ya mkoa wa Iringa na ambayo ni Iringa mjini ,Kilolo ,Kalenga na Ismani .

No comments:
Post a Comment