Sunday, May 27, 2012

JK kufungua mkutano wa AFBC unaotarajiwa kugharimu sh. Bilioni 12







Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDB wakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha Magonya  katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Arusha.



   Na Mwandishi Wetu Arusha
 Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete  huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea.
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha  Magonya  ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na faida kubwa sana.
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza Jumatatu ijayo utakuwa na faida kubwa sana kwa jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali kutoka katika maeneo ya nchi mbalimbali duniani watabadilishana hata uzoefu.
“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu sana hasa katika mchakato wa uchumi na kwa hali hii pia tunatarajia hata kufanya maendeleo mbalimbali  ikiwemo kufanya marekebisho kwa jengo la kimataifa la AICC”alisema Bw. Magonya.
Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza kuimarisha uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia kutumia fursa mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku malengo yakiwa ni kuendeleza uchumi kwa walengwa.
Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza uchumi pia benki hiyo ina mikakati mbalimbali ya kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama njia ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania.
Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa kujenga barabara ya Arusha – Holile ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo hasa ya mawasiliano.
Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema fursa za mkutano huo ili kuweza kuimarisha biashara zao za kila siku.

No comments:

Post a Comment