Friday, May 18, 2012

Nashangaa tunapotafuta vazi la taifa wakati tunalo tayari!

 

   NINAPOSEMA nashangaa taifa linapoingia katika mchakato wa kutafuta vazi la taifa wakati tayari tunalo.Kimawazo yangu nadhani mchakato wa kutafuta vazi la taifa si sahihi, kutokana na vazi hilo lipo hasa kwa wanawake kwani kila kona ninapopita nakutana na wanawake wakiwa ndani ya vazi hilo.Hapa kwa mtu wa kawaida ambaye ana mawazo kama ya kwangu anaweza kuungana nami kushangaa, hawa watu wanaodai kuwa wanatafuta vazi la taifa, kwa watu gani, kwani hatuna hadi hivi sasa, mbona tunalivaa muda wote? tena kwa kila mtindo ambao mhitaji anataka?
Kama hujui vazi hilo nakuambia kuwa ni KANGHA.hivi kuna sehemu yoyote mwanamke wa Kitanzania anaweza kwenda bila kuwa na KHANGA?.Jibu kama ndiyo, basi hatuna haja ya kutafuta vazi la TAIFA,labda kama wanalo lao jambo.
Hivyo, wito wangu kwa kamati ya mchakato wa vazi la taifa, nawaomba wasihangaishe saaana ubongo wao kutafuta vazi la taifa, kazi walisharahisiwa, aamueni kitu kimoja kutumia KHANGA kama vazi la taifa, mnapotucheleweshea kuhalalisha KHANGA kuwa vazi la Taifa hatuwaelewi.
Nadiriki kusema hivyo kwa sababu, gharama ya kununua KHANGA anaweza kumudu mwananchi yeyote yule,  kama ilivyo kwa hivi sasa, hivyo Khanga kuwa vazi la taifa sioni kama kuna ubaya wowote.

No comments:

Post a Comment