Na Mwandishi Wetu, Arusha
JAMII nchini imeaswa
kuachana na uchangiaji wa anasa badala yake ijikite zaidi kuyajali
makundi yasiyojiweza hususani watoto yatima na wenye maambukizi ya ukimwi
wanaolelewa bila msaada wa uhakika kwenye vituo vya watoto yatima .
Hayo yalisemwa jana na
mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano cha jijini Arusha,Bw .Godiliste Temba wakati
kikundi hicho kilipotembelea na kutoa msaada wa vyakula na vinywaji kwa vituo
viwili vya kulelea watoto yatima kikiwemo kituo Sant Lusia
kilichopo Moshono jijini Arusha ,kinacholea watoto wenye maambukizi ya ukimwi
pekee na kituo cha Sant Joseph kilichopo kata ya Mlangalini
wilayani Arumeru.
Bw Temba aliwaomba
watanzania kujijengea utaratibu wa kujisaidia wenyewe na kuachana
na dhana iliyojijenga ya kutegemea wafadhili pekee kutoka nje ya
nchi ambao wengi wao wamekuwa wababaishaji huku wakiweka masharti
magumu na misaada yao .
Aidha alisema
jamii inakila sababu ya kuguswa na tabu wanayoipata watoto yatima
kwani mbali na kukabiliwa na changamoto nyingi kimaisha wamekosa msaada muhimu
ya kijikimu hususani elimu bora itakayowasaidia kuondokana na utegemezi hapo
baadae.
Ametoa rai kwa kila
mtanzania kwamba jukumu la kuyasaidia makundi hayo ni wajibu wakila mtu
iwapo ataguswa nakujitolewa walau kuchangia mtoto mmoja kila mwaka
ikiwepo kumsombesha na kuachana na uchangiaji mkubwa wa anasa
ambao umekuwa ukipoteza fedha nyingi kwa muda mfupi
‘’suala la kuwasaidia
watoto ni jukumu la kila mtu ni vizuri basi kwa kila mtanzania iwapo ataguswa
kwa namna yake na kutoa mchango kwani wengi wetu tumekuwa tukijitoa sana
kuchangia harusi zakifahari,bila kujali kuwa michango yetu pia inahitajika kwa
makundi mengine muhimu’’alisema
Naye Mkuu wa kituo cha
watoto yatoma cha St.Lucia BiWinfrida Mrema,alisema kuwa kituo chake kinalea
watoto wenye umri wa miaka 2 hadi 10 wenye maambukizi ya VVU na kimekuwa
kikikabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa lishe bora kwa
watoto hao.
Aliwaomba wananchi
kuendelea kujitolea kuwasaidia watoto hao kwani wengi wao hawana wazazi na
wamekuwa wakiletwa kituoni hapo wakiwa kwenye hali mbaya ya maambukizi ya ukimwi
baada ya kutelekezwa na wazazi wao au baadhi wazazi
kufariki dunia na kuwaacha yatima bila msaada
.
Aidha kwa upande wa
mmiliki wa kituo cha St.Joseph Sister Crispin Mnate.. alisema kuwa
kituo hicho kina jumla ya watoto yatima 46 na wamekuwa wakilelewa katika
mazingira magumu kutokana na kukosa ufadhili wa kudumu.
Alisema changamoto
kubwa inayokikabili kituo hicho ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya
kuwalipia ada wanafunzi wanaosoma ndani na nje ya jiji la Arusha
chini ya uangalizi wa kituo hicho wakiwemo wawili wanaosoma shule
za sekondari.
Alisema amekuwa
akipokea watoto wachanga wanaozaliwa na wazazi wao kisha
kutelekezwa ama kutupwa majalalani na kuwaanzishia huduma ya matunzo hadi
kufikia umri mkubwa ,hivyo alidai kuwa uwezo wa kumudu kuwahudumia watoto hao ni
mdogo na kuwataka watu binafsi ,mashirika ya umma na taasisi mbalimbali
kujitokeza kusaidia vituo hivyo vya kulelea watoto
yatima.
No comments:
Post a Comment