Lulu
(katikati) akiingia mahakamani na askari magereza wa kike.
Hapa ni
karibu na mlango wa kuingia katika chumba cha mahakama.
Msanii
wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena
kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo
mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la
kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa
mahakamani hapo.
Fungamtama
na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama
ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa
mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina
mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na
mshitakiwa huyo.
No comments:
Post a Comment