Na Mwandishi wetu, Shinyanga.
Wanachama wa Chama cha kutetea
haki za wanaume wanaonyanyaswa na wake zao Tanzania wamekutana katika
kikao cha dharura mjini Shinyanga kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni
pamoja na mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba na usajili wa Chama hicho
chenye lengo la kuwatetea wanaume nchini wanaokabiliwa na manyanyaso
dhidi ya wake zao.
Kikao hicho ambacho kimefanyika
katika Hoteli ya Karena mjini humo,Katibu wa chama hicho Bw.Antony Sollo
amesema Chama hicho kinatarajiwa kusajiliwa na kuzinduliwa rasmi mapema
Julai mwaka huu hapa nchini na kwamba tayari hadi hivi sasa wanaume
waliowengi wamekipokea na kuonesha dhamira ya kujiunga.
Amesema kuunda kwa Chama hicho
kumetokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya wanaume nchini wamekuwa
wakinyanyaswa na hawana mahali pa msaada kwao hatua ambayo imekuwa
ikiendelea kuwafanya kuwa wanyonge katika kukabiliana na matatizo ya
manyanyaso waliyonayo.
Katibu huyo Bw.Sollo amefafanua
kuwa vitendo vya manyanyaso kwa wanaume hapa nchini pia vimekuwa
vikisababisha mauaji ya mara kwa mara na hata kuleta mfarakano ndani ya
familia.
Amesema kuanzishwa kwa chama hicho
pia kutasaidia kuimarisha mahusiano baina ya wanandoa kwakuwa wataishi
kwa usawa huku wakizingatia haki na wajibu wa kila mmoja wao katika
maisha ya kila siku.
Kwaupande mwingine mwenyekiti wa
chama hicho Bw.Belensi amewataka wanaume nchini kukiunga mkono chama
hicho ambacho kitakuwa ni kimbilio la wanaume na pia msaada kwa ngazi ya
familia kutokana na migogoro inayojitokeza ndani ya ndoa.
Miungoni mwa Masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kero ya wanaume kudharauliwa, kupigwa na wake zao kila siku na baya zaidi ni pale wanaponyimwa haki ya ndoa.
Mengine ni yanayohusu wanawake kubadili na kumiliki haki na mali walizochuma pamoja na wenzi wao hatua ambayo pia imeonekana kikwazo kwa wanaume.
Huu ulikuwa ni mkutano wa pili tangu kuanzishwa kwa mchakato wa chama hicho jijini Dar-es-salaam.
Pichani ni Afisa habari wa Kituo cha kutetea haki za binadamu (LHCR) Bi. Rose |
Pichani ni baadhi ya waangalizi wa haki za binadamu wakiwa wanamsiliza kwa makini mkufunzi wa semina hiyo hayuko pichani, katika mafunzo ynaayoendelea mjini Shinyanga katika hoteli ya Karena.
Shinyanga
KUTOKANA na Katiba ya sasa kukabiliwa na upungufu mkubwa, kituo cha Sheria na kutetea haki za binadamu (LHRC) kimedhamira kupigania ili mambo kadhaa kama elimu iingizwe katika katiba mpya ili iwe haki ya msingi za binadamu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwezeshaji kutoka katika kituo cha kutetea haki za binadamu, Bi. Laetitia Petro wakati akiwasilisha mada iliohusu Chimbuko la Haki za Binadamu nchini Tanzania kwa waangalizi wa haki za Binadamu kutoka katika mikoa za Mwanza, Kagera, Kigoma, Mara,Tabora na Dodoma kinachoelendea katika ukumbi wa Hoteli ya Karena mjini Shinyanga.
Bi. Petro ambaye pia ni Wakili na Mwanasheria alisema katiba ya sasa inayo upungufu mkubwa hasa katika suala ya nzima ya ulinzi wa haki za binadamu.
Alisema licha ya elimu ni ya msingi katika maisha ya haki za binadamu, lakini katiba ya sasa haioneshi msisitizo wake kwa wananchi.
Alisema haki zingine ambazo hazimo kabisa katika katiba ya sasa ni pamoja na haki ya kupata maji safi na salama haki ya mazingira masuala ambayo ni ya msingi katika ustawi wa haki za binadamu katika kizazi kijacho.
No comments:
Post a Comment