Sunday, May 27, 2012

Taifa Stars, Malawi zaingiza Mil. 40/=


Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 40,980,000.
Mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000. Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).
 

No comments:

Post a Comment