Monday, May 21, 2012

Miaka 16 kuzama kwa Meli ya MV. Bukoba, Rais wetu JK iko wapi Meli uliowaahidi wananchi wa Kanda ya Ziwa?

Meli ya Mv Bukoba ikizama Mei 21,1996 ikiwa imebakiwa takribani kilomita nane kutia nanga katika bandari ya Jijini Mwanza.
Mnara wa kumbukumbu ya abiria waliozikwa Jijini Mwanza
 LEO mei 21, 2012 tunakumbuka ajali mbaya ya MV Bukoba ilikozama katika ziwa Victoria miaka 16 iliopita.Ni siku ambayo ni vigumu kufutika ndani ya akili za Watanzania walio wengi hasa waishio Kanda ya Ziwa.Ni siku ambayo mtu akikumbuka kwa kweli humpatia wakati mugumu kuendelea kuishi hapa duniani.Lakini yote tumaliza kwa kumuomba Mungu atupatie nguvu na faraja hasa kwa wale waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.
Lakini swali la kuhoji i.. wapi meli alioaahidi Rais Jakaya Kikwete mwaka 2010, kwani miaka inavyokwenda, huku akikaribia kuachia ngazi, wananchi wanaingiliwa na wasi wasi wa kutimizwa kwa aahadi hiyo.

No comments:

Post a Comment