Tuesday, December 4, 2012

Wanaharakati wa mazingira wakutana Doha

Bi Blandina Cheche na Dkt Fadhila Khatib kutoka Baraza la taifa la hifadhi na usimamaizi wa mazingira NEMC wakifuatilia mawasilisho toka kwa wenyeviti wa kamati mbalimbali kwa Rais wa COP 18 hawapo pichani
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira mh.Dkt Terezya Huvisa, katikati aliyekuwa waziri wa mazingira nchini Uganda mh. jesca eriyo katikati na bi wivine ntamubano afisa mazingira mkuu kutoka wizara ya mazingira nchini Burundi katika briefing ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kwa upande wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki
kutoka kushoto katibu mkuu wizara ya mazingira kenya bw ali mohamed,waziri wa mazingira znz mh fatma ferej, katibu mkuu ofisi ya ya makamu wa kwanza wa rais znz dkt omar dadi shajak,mkurugenzi mazingira ofisi ya makamu wa rais Jkt Julius Ningu na katibu mkuu ofisi ya  makamu wa rais bw sazi salula katika briefing ya jumuiya ya afrika mashariki inyohusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi .picha zote na evelyn mkokoi
Wadau wa Mazingira wamekutana leo na kupata mawasilisho kwa ufupi kutoka kwa Mh. Jessa Eriyo, aliyewahi kuwa waziri wa mazingira nchini uganda ambae kwa sasa  ni Deputy Secretary general in change of productive and sociol sectors katika jumuiya ya afrika mashariki.
 
Bi. Eriyo,amesema suala la mabadiliko ya tabia nchi ni agenda ambayo imekuwa ikijadiliwa tangu mwaka 2009 katika jumuiya ya afrika mashariki, na kwa upande wa utekelezaji jumuiya imefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na ku sign makubaliano ya kifedha ya miaka mitano ya miradi ya mabadiliko ya tabia nchi.
 
Aliongeza kuwa kuna program ya miaka mitano ya kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo italenga zaidi katika kuwa na kilimo enendelevu.alisema kuwa Mkakati wa jumuiya wa mabadiliko ya tabia nchi pia unaendelea kufanyiwa kazi na kuwa sambamba na suala zima la mabadiliko yatabia nchi jumuiya pia inalifanyia kazi suala la maji.
kwa ufupi ni hayo kwa mida hii bado nahudhuria mikutano mingine nitaleta yaliyojiri,nawashukuru kwa ushirikiano

No comments:

Post a Comment