Na
Theonestina Juma, Kagera
UMOJA wa
makanisa ya kikristo mkoani Kagera umesema hawafurahishwi na hali halisi
inayoendelea hapa nchini na kwamba, jibu pekee ni wananchi kumrudia Mungu na
kutoruhusu kugombanishwa na ukoloni mamboleo.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Mratibu wa siku ya maombi ya kuiombea taifa usiku wa mkesha wa mwaka mpya unaotarajiwa kufanyika Desemba 31,mwa huu katika uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 12 jioni hadi saa 6 usiku, Mchungaji wa kanisa la
Tanzania Fellowship of churches Jijini Dar Es Salaam, Paulo Kashaga
wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa juu ya maandalizi
ya siku hiyo.
Alisema
“kamwe sisi viongozi wa dini hatufurahishwi na mambo yanayoendelea hapa nchini,
ya kuchomewa makanisa, viongozi wa dini kupigwa risasi, kumwagiwa
tindikali,haya mambo hayakwepo hapo awali hapa nchini mwetu, …. Kwa sasa
yanatengezwa (artificial), yanachochewa
na ukoloni mambo leo, viongozi wa dini nao wasilikubali hili”.
Kutokana na
kutofurahishwa na vitendo hivyo, tayari baadhi ya viongozi wa dini katika
nafasi zao wameshaandika barua nyingi na kuziwasilisha serikali kwa kutoa
mapendekezo yao nini kifanyike na hii ni kutokana na mambo mengine yanayohitaji
marejeo.
Mchungaji
Paulo ambaye kitaalum ni mhandishi na ni
mwanajeshi Mstaafu (JWTZ), alisema waumini wa kikristo na wananchi kwa ujumla
kamwe wasikubali kuyumbishwa na ukoloni mambo leo, ambayo yanaingilia kupitia
kuwagombanisha watanzania kidini ili waweze kupata nafasi ya kuchuma maliasili
ya nchi.
"Malumbano
yanayoibuka kwa sasa hapa nchini ni kutokana na kugombanishwa, na kama
watalitambua hilo na kukataa kugombanishwa wagombanishaji hao hawawezi
kufanikiwa na pia yanatokana na watu kuacha maadili ya ki-Mungu na kutawaliwa na utandawazi ambayo
nchi haiwezi kukwepa”alisema mchungaji huyo.
Mchungaji
Paulo alisema maombi pekee kwa wakristo ndiyo silaha kubwa ya kutunza
amani na utulivu wa nchi yetu.
Alisema
lengo la kuendesha maombi hayo mkesha wa mwaka mpya ni kwa ajili ya
kuiombea nchi amani na utulivu, watawala
na vyama vya siasa pamoja na bunge letu, kwa sababu hawataki masuala ya malumbano yakitokea bungeni ambako
ndiko tegemeo la nchi katika kutunga sheria, na kwamba maombi hao yatafanyika katika mikoa 17 ikiwemo na Zanzibar
Akizungumzia
juu ya maandalizi hayo, alisema yamekamilika kwa asilimia 100 kutokana na watu
wengi pamoja na wafanyabiashara wa mjini hapa wamehamasika kutoa sadaka zao kwa
kuchangia uendeshaji wa mkesha huo na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa
uwingi kushiriki katika maombi hayo
Alisema siku
ya mkesha wa mwaka mpya, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa Kagera,
Kanali Fabian Massawe na kwamba yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Kuhusu
malalamiko yanayotolewa baadhi ya viongozi kwa kuwa inapendelea dini fulani,
mchungaji huyo aliwataka kuachwa kabisa kwa sababu hayana busara kwani serikali
inayokuwa madarakani Mungu anaitambua
halijaishi kama kiongozi ni Muislamu ama mkristo .
“Mimi
nawaomba viongozi wa dini ,Maaskofu, mashekhe waachane kusema maneno ya upendeleo kwani hayana busara
kabisa , hayampendezi Mungu, tunawaomba Watanzania wananchi kama nchi moja ,
dunia inatuangalia sisi kama tuna
ukombozi, kwani tunayo madini na rasilimali zetu, mfano kama Geita hawajui zile
dhahabu zimetoka wapi”alisema
Mwisho.
No comments:
Post a Comment