MWIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando na
mwenzake Enock Jonas (Zunguka) wanatarajiwa kuutikisa mji wa Bukoba katika
tamasha la kwanza kubwa kufanyika Mkoani Kagera.
Akizungumzia tamasha hilo Rose amesema
amejiandaa kusherekea Uhuru kwa aina yake tofauti na watu wengi walivvozoea kwa
kuwashirikisha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira
magumu.
Nimefurahi kupata nafasi ya kutumbuiza
katika tamasha hili la aina yake hasa katika mkoa wa Kagera ambapo itakuwa mara
ya kwanza kuonekana live katika mji wa Bukoba.
Nawaomba wananchi wa Bukoba kufika kwa
wingi katika tamasha hili la kipekee katika ukuonyesha moyo wa upendo
kushirikiana na kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.
“Nimejiandaa kuwapa nyimbo mpya ambazo
bado hawajawahi kuzisikia,itakuwa mara ya kwanza kuziimba katika tamasha
hili.alisema
Tamasha hilo la Shangwe Kagera lina lengo
la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi
katika maisha magumu.
Wakati huohuo Enock Jonas ‘Zunguka’
wamewataka wakazi wa Kagera kukaa sawa kwa ajili ya tamasha hilo na watarajie
kupata burudani ya kutosha na ya kipekee kutoka kwake ambayo itawajenga roho ya
imani, kupendana na kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi katika mazingira
magumu ili nao waweze kufaraia maisha.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula
Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta anasema
kuwa matayarisho ya tamasha hilo yanaendelea vizuri kutokana na mwitikio mkubwa
wa watu mbalimbali waliojitokeza kushiriki.
Pia, Mutta anasema bendi ya muziki ya
wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya wa makanisa
mbalimbali, kikundi cha watoto yatima wamejitokeza pia kutumbuiza.
“Mpaka sasa tumekamilisha sehemu kubwa
ya matayarisho hayo na tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika maeneo yote ya mji
wa Bukoba nje ya mji” alisema.
Lengo la Tamasha:
Ni kuhamasisha jamii kuishi kwa
amani,kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza kimaisha ili na wao
wajione ni sehemu yao.
Katika kutambua hilo kampuni yetu
iliamua kufanya utafiti mdogo nakugundua changamoto nyingi katika Mkoa wa
Kagera, mojawapo ni kuwa na watoto wengi wanaoishi katika mazingira magumu.
Baada ya kuliona hili, tulitembelea vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao,
mojawapo ni Tumaini Children’s Centre kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la
Ki lutheri Tanzania (KKKT).
Kituo hiki kinalea watoto wote bila
kujali kabila,jinsia wala dini zao, kwa sasa kituo hiki kinahudumia watoto
zaidi ya 800, kwa kuwapatia elimu,chakula, malazi n.k ambapo kwa muda mrefu
kimekuwa kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa wametangaza kuusitisha kwa
maelezo kuwa jamii ya Watanzania inapaswa kujifunza na kuanza kuhudumia watu wao
wenyewe.
No comments:
Post a Comment