Monday, December 24, 2012

Uzinduzi wa albam ya Yesu ni mwema wa Kapotive wafana Bukoba, kivutio kikubwa ni Padri Anthony Musaala wa Uganda na Christina Susho

 Familia ya Dr. Kalumuna ilikuwa miongoni mwa walioudhuria uzinduzi wa albamu ya yesu ni mwema uliofanywa na kundi la Kapotive star singers uliofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya Linas ulioko mkoani Kagera katika manispaa ya Bukoba.
 Askofu msaidi wa jimbo la Bukoba, Dkt. Methodius Kilaini akibadilishana mawazo na baadhi ya watu kabla ya uzinduzi wa albamu ya yesu ni mwema.
 Kwaya ya kanisa katoliki ya kikango cha Rwamishenye ikitumbuiza kabla ya  uzinduzi wa albamu ya yesu mwema.
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya utalii ya Kiroyera, Mary Kalikawe alikuwa miongoni mwa walioudhuria uzinduzi wa albamu ya yesu mwema, anaonekana akijadiliana jambo na mmoja wa marafiki zake.
 Kwaya ya vijana ya kanisa la kiinjili la kilutheri la dayosisi ya kaskazini magharibi ikitumbuiza.


 Kikundi cha kwaya cha kanisa la SDA nacho hakikubaki nyuma wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo.
 Kikundi cha nyimbo za injili cha The Groover  parokia ya OLD Kampala nchini Uganda katika  kinachoongozwa na Padre Anthony Musaala  kikifanya vitu kabla ya uzinduzi wa albam, padre Musaala aliwakuna watu alipoimba wimbo unaotamba wa injili wa ampeche a mgongo.
 Padrei Musaala akiimba sambamba na walioudhuria uzinduzi wa albamu.
 Akiimba sambamba na kundi zima la Kapotive star singers.
 Kundi la Kapotive star singers likifanya vitu wakati likitambulisha albamu kiliyoizindua rasmi ya yesu ni Mwema, uzinduzi wa albamu hiyo ulifanyika jana, kwenye ukumbi wa klabu ya linas na kuhudhuliwa na maelfu ya watu.
 Mambo ya kundi la Kapotive star Singer, kundi hili linaitaji zaidi ya shilingi zaidi ya milioni 32 kwa ajili ya kufanikisha shughuli yake ya kurekodi albamu mbalimbali kinachotaka kusisambaza, usiku wa uzinduzi wa albamu jumla ya shilingi zaidi ya milioni 15 zilipatikana.

No comments:

Post a Comment