Na
Theonestina Juma, Kagera
WAKATI
baadhi ya Makamanda wa Jeshi la polisi wakipiga marufu ya disko toto, kwa mkoa
wa Kagera hali iko tofauti kutokana na kuruhusiwa kuwepo nyakati za sikukuu
Kamanda wa
polisi Mkoa Kagera, Phillip Kalangi akizungumza na waandishi wa habari alisema
disko toto linaruhusiwa nyakati za sikukuu mkoani Kagera ambapo waandaji
wanatakiwa kufuata utaratibu na maagizo yaliotolewa na Jeshi hilo.
Alisema
wandaaji wa disko toto wanatakiwa kuaandaa sehemu ambayo iko wazi, ambayo
haiwezi kuhatarisha maisha ya watoto.
Alisema watu
hao wanatakiwa kuwa na kibali maalum kwa wale wanaoaandaa disko toto.
Alisema
sababu ya kuhjitaji swehemu ambapo pako wazi ni kutokana na baadhi ya maeneo
kutokuwa na miundo mbinu.
“Maeneo ya
kufanyia disko toto lazima pawe pawazi ili likitoea tatizo lolote linakuwa
rahisi kutoa msaada na watoto wasijazwe kupita kiasi, lazima muandaaji awe na
kipimo, idadi ya watoto aliowalenga’alisema.
Hata hivyo
katika uchunguzi wa gazeti hili katika kata ya Katoma kuliezewa kumbi kwa
kutumia makuti kwa ajili ya kuendeshea disko toto.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment