Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Kikwete amefanikiwa kufanya mazungumzo na Rais wa zamani wa
Madagaska Marc Ravalomanana ambaye amekubari kurudi nchini kwake baada ya kuwa
uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2009.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya
habari Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Raisi Kikwete amesema Ravalomanana amekubali
pia kutokugombea katika uchanguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Mei 2013 ili
kuleta amani na utulivu.
“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na
amekubali kurudi nchini kwake madagaska na kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi
za
Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya
hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.
Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska bila masharti yoyote
na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo ikisaidiana na Jumuiya ya
SADC.
Kwa upande wake Rais Ravalomanana
amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo na
amesema anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia
Madagaska kuwa katika hali ya amani.
“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa
kufanikisha mazungumzo haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga,
kuimarisha na kushirikiana na wananachi
ili kuleta amani na utulivu,” amesema
Ravalomanana.
Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika la kufanya mazungumzo na Marais wote wa
wawili, Rais wa sasa wa Madagaska
Andry Rajoelina na
Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande
wa Rais Rajoelina.
No comments:
Post a Comment