Mc’s wa
Onyesho la Mavazi la Red Ribbon Fashion Gala 2012 Abby Plaatjes na Evance Bukuku
wakikaribisha wageni na kutoa utaratibu wa shughuli nzima katika Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Mwanamitindo wa Kimataifa nchini na Balozi wa
Tanzania Mitindo House (TMH) Flaviana Matata akifungua maonyesho hayo na vazi la
Ubunifu wa Khadija Mwanamboka.
Pichani
Juu na Chini ni Models wakionyesha mavazi mbalimbali yaliyobuniwa kutokana na
Vitenge vilivyotengenezwa na Kiwanda cha Vitenge cha Morogoro Polytex ambacho ni
moja wapo ya Makampuni ya MeTL.
Msanii wa
muziki wa Kizazi kipya Linex akiimba wimbo maalum wa kuhamasisha jamii kusaidia
watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwenye onyesho la Tanzania
Red Ribbon Fashion Gala 2012.
Muasisi
na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House Bi. Khadija Mwanamboka (kulia)
akimkabidhi cheti ushiriki kwa Meneja Masoko wa CFAO MOTORS Tharaia Ahmed
(katikati).
Mwakilishi wa Kiwanda cha 21 CENTURY TEXTILE
kinachotengeneza vitenge vya Morogoro Polytex kilicho chini ya Kampuni za
Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa akipokea cheti cha
ushiriki kutoka kwa Bi. Khadija Mwanamboka.
Morogoro
Polytex ni kiwanda cha kuzalisha vitenge na chenye uwezo wa kuzalisha mita
milioni 100 kwa mwaka na ndicho kiwanda kikubwa kwa sasa katika ukanda wa eneo
la Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Flaviana Matata Foundation Bi.
Flaviana Matata akipokea cheti cha heshima kwa kushiriki kwenye onyesho la
Tanzania Red Ribbon Fashion Gala 2012 ambalo limefanikiwa kukusanya kiasi cha
Shilingi Milioni 72 kwa ajili ya kuwasaidia na kuwaendeleza watoto yatima wa
kituo cha TMH wakiemo wenye kuishi na virusi vya
Ukimwi.
Omari Salisbury wa Qway International
wanaosambaza vinywaji vya Belvedere Vodka akikabidhiwa cheti kwa
mchango wao kutambuliwa na TMH.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer
Wines & Spirits Ltd – Benedicta Rugemalira akitabasamu baada ya kupokea
cheti kutokana na kampuni yake kutoa mchango mkubwa katika kuwezesha ufanisi wa
shughuli ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kituo cha watoto yatima cha
TMH ambapo kampuni yake Mabibo Beer Wines & Spirits ilihusika kikamilifu
kunywesha wageni.
Wanamitindo Flaviana Matata na Jennifer Bash
wakipita jukwaani na magauni yaliyotengenezwa na mbunifu wa kimataifa Sherri
Hill wakiyanadi kwa wageni kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kituo cha
watoto yatima cha TMH.
MC Evance
Bukuku akinadi gauni lililovaliwa na Mwanamitindo Jennifer Bash lililobuniwa na
Sherri Hill.
Wanamitindo wakionyesha magauni hayo meza kuu ya
wageni waalikwa akiwemo Mh. Zitto Kabwe.
Wageni
waalikwa waliotia fora katika maonyesho hayo ambao walinunua magauni ya Sherri
Hill kwa shilingi Milioni 4.8 Anitha (Kushoto) na Milioni 4 Alma ( wa pili
kushoto) ikiwa ni mchango wao katika onyesho la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala
2012.
Mwakilishi wa Mohammed Dewji Foundation Bw.
Cosmas Mtesigwa akinunua bidhaa za mnada zilizotoka kwa mmiliki wa Kampuni ya
Diamond Empowerment Fund Russel Simmons wa nchini Marekani zenye thamani ya
shilingi Milioni 5 ikiwa ni mchango wa Mohammed Dewji Foundation kwa kituo cha
watoto yatima cha TMH.
Mh. Zitto
Kabwe akionyesha kitabu ‘SUPER RICH’ kilichoandikwa na Russel Simmons
alichonunua kwa thamani ya Shilingi Milioni 4 kama mchango wake kwa kituo cha
watoto yatima kinachoongozwa na Mwanamitindo Khadija Mwanamboka cha TMH. Kushoto
ni Mwanamitindo wa Kimataifa Mtanzania anayeishi nchini Marekani aliyekuja na
bidhaa hizo Flaviana Matata.
Flaviana
Matata akiwaonyesha wageni baadhi ya bidhaa alizokuja nazo kutoka kwenye kampuni
ya Diamond Empowerment Fund ya Russel Simmons ya nchini Marekani ambao ni
mchango wa mfanyabiashara huyo wa kimataifa kwa kituo cha
TMH.
Mh. Zitto
Kabwe na Chief Judge wa BSS Madam Ritha Paulsen katika Meza
kuu.
Flaviana
Matata na Eve Collection.
Mwakilishi wa Kampuni ya MeTL Cosmas Mtesigwa
(kulia) Operation Manager wa Mo Blog Johary Kachwamba na Assistant Operation
Manager Zainul Mzige nao waliokuwa miongoni mwa wageni
waalikwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer
Wines & Spirits Ltd Bi. Benedicta Rugemalira akiwa na binti yake mmiliki wa
Eve Collection.
Mh, Zitto
Kabwe sambamba na msanii Linex wakichana mistari ya wimbo wa Lekadutigite katika
hafla hiyo.
Hafla
hiyo ilipochanganya…… Shose Sinare naye alishindwa kujizuia na kujiunga na Mh.
Zitto Kabwe na Msanii Linex katika Lekadutigite.
Tharaia
Ahmed wa CFAO MOTORS (katikati) akishow love na wadau.
Mc Abby
Plaatjes na wadau.
No comments:
Post a Comment