Mwanamke wa kweli
mwenye moyo wa umama ametofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamke
mwingine yeyote. Mwanamke huyu awe amebarikiwa kupata watoto ama la
lakini atakuwa na sifa zifuatazo.
1) Ana upendo wa kweli kwa watu wa nyumbani mwake. Yaani si mbaguzi
hata kidogo.Na daima huifanya familia yake kuwa priority. Na kwamwe
hutumika kama daraja la kuunganisha familia zote mbili alikotoka yeye na
alikotoka mumewe.
2) Ana hekima katika kuyakabili mambo ya nyumbani mwake. Hata siku moja
haamui mambo kwa ujinga na daima busara yake ndio silaha yake.
3) Ana uvumilivu sana katika jambo lolote lile gumu na daima huona gumu lolote limpatia kama changa moto tu na si kama kosa.
4) Ana siri sana juu ya maisha ya nyumbani kwake daima hukuti mambo ya nyumbani nje watu wakiyajadili.
5) Ni mchapa kazi hodari, tena ambaye hawezi kuruhusu familia yake
ikalala njaa kisa baba hajaleta chakula. Ama watoto wasisome shule kisa
baba hajalipa ada.
6) Daima ni muaminifu na anaaminika sana kwa matendo yake.
7) Siku zote huamka wa kwanza nyumbani, na hulala wa mwisho. huakikisha mambo yote ya ndani yako sawa kabla ya yote.
8) Huwa hadekezi watoto wala haengi watoto katika kazi,huakikisha
nyumbani kwake kila mtoto ni mchapa kazi na nidham ya ndani ya nyumba
ipo.
9) Si mbishi wala hawezi kubishana na mumewe mbele za watu, kwani ni
msikivu sana kwa mumewe na daima humfanya mume kuwa kiongozi na kamwe
huwa habadili cheo cha baba.
10) Ni mwepesi wa kukiri makosa yake kwa mumewe na kuomba samahani lakini pia ni mzuri sana kwenye kuremedy makosa yake.
13) Siku zote ni msafi wa mazingira na mwili daima nyumba yake husifika kwa usafi.
14) Mume na watoto wake hujulikana hata wanapoonekana njiani maana yake
huakikisha amewavesha vizuri, kinadhifu na watoto wanaheshima sana.
15) Ni mcha Mungu, kwa imani yake. hata kama baba si mtu wa sala lakini yeye huongoza watoto katika ibada kila iitwapo leo.
16) Hupendelea zaidi maendeleo hasa ya kiuchumi na daima hupenda vitu vizuri na hujitahidi sana vipatikane.
17) Si mpayukaji wala mtu wa kisirani nyumbani mwake. Maneno yake huwa
yaliyopangiliwa kwa sauti yenye kunyesha mamlaka lakini yenye upole.
18) Hupendelea kupika na hujisikia furaha sana akipika kwa ajili ya
familia yake. Na siku akipika basi hata watoto husema leo tunakula
chakula kitamu manake ni desturi yake kupika chakula kitamu.
19) Humuheshimu sana mumewe, na daima hupenda kuisikia kauli ya mumewe
katika maamuzi. siku zote humfanya baba kuwa msemaji wa familia yake na
huakikisha kauli ya baba inatekelezwa.
20) Kamwe huwa hana dharau, wala majivuno, wala kiburi, wala uchoyo wala unafiki kwa mtu yeyote yule.
Chanzo jamiiforums
No comments:
Post a Comment