Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kulia) akimuonyesha
Victoria Zitta Mnyanyi (kushoto) ambaye ni Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu
cha Mzumbe tawi la Mbeya moja ya nyumba ya kale iliyokuwa inatumiwa na kabila
la wasafwa ambalo ni kabila maarufu mkoani humo. Mponzi ameamua kujitolea
kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ambacho kitatunza kumbukumbu za
utamaduni na mila zote ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na
mababu zao.
(PICHA NA ANNA NKINDA MAELEZO-DAR ES
SALAAM)
Baadhi ya wakazi wa Mwasanga jijini Mbeya wa kabila la wasafwa
wakimuangalia Mary John akisaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe aina ya “Lwala”
wakati walipotembelea ili kujionea ujenzi wa kituo cha utamaduni wa kabila lao
kinachojengwa kwa kujitolea na Sosteli Mponzi. Baadhi ya wasafwa waishio
maeneo ya vijijini bado wanasaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe hilo kwa ajili
ya kutengenezea pombe.
Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kushoto)
akimuonyesha Victoria Zitta Mnyanyi ambaye ni mshauri wa wanafunzi wa chuo
kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya mti wa asili aina ya msulusulu ambao wazee wa
kabila la wasafwa walikuwa wakiutumia kwa ajili ya kutibu mifugo. Mponzi ameamua
kujitolea kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ili kumbukumbu zisiweze
kupotea kwani hivi sasa kutokana na utandawazi makabila mengi yamekuwa
yakipoteza utamaduni wao.
Baadhi ya wakazi wa Mwasanga jijini Mbeya wa kabila la wasafwa
wakicheza ngoma aina ya Mbeta ya kabila hilo ambayo inachezwa wakati wa kumaliza
msiba “Mwengulo” kama walivyokutwa na mpiga picha wetu hivi karibuni
alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila la wasafwa. Ujenzi
wa kituo hicho unajengwa kwa kujitolea na Sosteli Mponzi ili kizazi kijacho
kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Hapa wakicheza ngoma ya kabila hilo ambayo inachezwa wakati wa
sherehe kubwa za kitaifa kama sabasaba na mwaka mpya kama walivyokutwa na mpiga
picha wetu hivi karibuni alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za
kabila la wasafwa.
Baadhi ya wakazi wa Mwasanga jijini Mbeya kutoka kabila la
wasafwa wakimwonyesha mpiga picha wetu jinsi wazee wa zamani wa kabila hilo
walivyokuwa wanakunywa pombe aina ya Kimpumu wakati alipotembelea kujionea
ujenzi wa kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila hilo.Kutokana na kuenea
kwa magonjwa mbalimbali ya kuambukiza hivi sasa kila mtu anakunywa pombe hiyo
kwa kutumia chombo chake.
No comments:
Post a Comment