Maziko hayo yametawaliwa na simanzi kubwa katika kijiji cha Kiterere kata ya Bukwe wilayani Rorya, ambapo aliendesha misa ya maziko hayo ni Padri kutoka katika Kanisa Katoliki parokia ya Kowak.
Mumewe Bi. RYOBA , BW.Charles Gibore,amesema kifo cha mkewe kimegubikwa na utata mwingi , pamoja na mambo mengine alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt Edward Hoseah(pichani) na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kubaini ukweli.
“Mke wangu aliuawa na mfanyakazi mwenzake na
tukio hilo limegubikwa na utata ambao Takukuru na Polisi ndiyo pekee wanaoweza
kutupa ukweli,” alisema Gibore nje ya chumba cha kuhifadhi maiti katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam.
Gibore alieleza kuwa mkewe huyo aliuawa usiku wa
kuamkia Jumapili katika tafrija ya kuagana na kupongezana na baadhi ya
wafanyakazi wenzake wa Takukuru waliokuwa wamepandishwa vyeo, tafrija ambayo
Bhoke alipewa zabuni ya kupika chakula.
Alisema pia mkewe aliombwa pia awapatie wenye
sherehe hiyo, vijana wawili wa kuwachomea nyama… “Vijana hao walikwenda asubuhi
ukumbini ili kuandaa eneo la kuchomea nyama, huku Bhoke akiwa bado nyumbani
akiandaa chakula,” alisema Gibore na kuongeza:
“Wale vijana walinieleza kwamba baadaye saa 8:30
mchana, Bhoke na wenzake walifika ukumbini na kuwakuta vijana wawili wanaofanya
nao kazi wakinywa pombe, huku wakichezea silaha aina ya bastola kujaribu
shabaha.”
“Vijana hao walifyatua risasi juu na ndipo muuaji
alipompiga kichwani marehemu katika jicho na mauti yalimfika muda mfupi,”
alisema.
Alisema baada ya hapo muuaji huyo alitoweka kisha
kujisalimisha mwenyewe katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Temeke,
Chang’ombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,
Engelbert Kiondo alithibitisha mtuhumiwa huyo kujisalimisha na kisha kushikiliwa
kituoni hapo na kueleza kuwa amekuwapo hapo Jumamosi iliyopita.
Kamanda Kiondo alisema pamoja na mtuhumiwa huyo
kujitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Takukuru, polisi wanaendelea kuchunguza ili
kubaini ukweli wa taarifa hizo.
“Tunaendelea kumshikilia hapa na uchunguzi
utakapokamilika tutamfikisha mahakamani kwa taratibu nyingine za kisheria,”
alisema Kiondo.
Marehemu Bhoke Ryoba alizaliwa Juni 18, 1978
katika Kijiji cha Kiterere, Wilaya ya Tarime mkoani Mara na anatarajiwa kuzikwa
kesho kijijini kwao. Ameacha watoto watatu; Doloresy (10), Dolrisy (4) na
Dolrick Gibore ambaye ana mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment