Mwanamuziki wa muziki wa
kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa
matibabu aliompatia ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth
Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.
---
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya
Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati
alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema aliyefuatana na Mama
yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya
yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za
mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa
kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango
kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa
na Rais.
(Picha na Freddy Maro
Ikulu)
No comments:
Post a Comment