Monday, December 31, 2012

Funga mwaka Kagera, mwalimu ajitia kitanzi kisa msongo wa mawazo



Na Theonestina Juma, kyerwa
MWALIMU wa shule ya msingi Mushisho Wilayani Kyerwa  mkoani  Kagera amejinyonga kwa kujitundika juu ya mti na kuacha ujumbe uliosema kuwa amechukua hatua hiyo kutokana na msongo wa mawazo yanayomkabili.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa polisi mkoani kagera, Phillip Kalangi tukio hilo limetokea Desemba 30, mwaka huu saa 4 asubuhi wilayani humo.
Mwalimu aliyejinyonga kwa msongo wa mawazo amejulikana kwa jina la Medadi Rwabiga ambapo jana hiyo alionekana akiwa amejitundika kwenye mti uliokuwa karibu na nyumba yake.
habari zinadai kuwa wakati mwalimu huyo alichukua uamuzi wa kujitia kitangazi, mke na watoto wake walikuwa wameenda kanisani. 
Imeelezwa kuwa tukio kama hilo la mwalimu huyo kutaka kujiua kwa kujinyonga si mara ya kwanza, kwani mapema mwezi Desemba mwaka jana alifanya jaribio la kutaka kujiua kwa kunywa dawa ya kuoshea mifugo.
Hata hivyo katika jaribio hilo mwalimu Rwabiga hakufanikiwa kujiua kwani aliwahishwa hospitalini na kupewa dawa na kuondoa sumu aliokuwa amekunywa kwa muda huo.
Hata hivyo katika kuonesha kuwa bado alikuwa na dhamira hiyo ya kutaka kujiua ilitimia hapo jana alipoamua kuchukua kamba na kutundika juu na mti na kujinyonga.
Habari zaidi zinasema kuwa mwili wa mwalimu huyo ulichelewa kuondolewa katika eneo la tukio, kutokana na  tatizo la daktari kupatikana mara moja.
Hata hivyo  kwa upande wa Kamanda Kalangi alisema hadi sasa hawajajua chanzo kilichomfanya mwalimu huyo kuchukua jukumu hilo nzito la kujinyonga na kwamba bado uchunguzi unaendelea.
“Jana kulikuwa na tatizo la daktari na hivyo leo Desemba 31, mwaka huu ndiyo daktari amepatikana na tayari polisi wako katika eneo la tukio kuufanyia uchunguzi mwili wa daktari”alisem na kwamba mwalimu Rwabiga ameacha watoto wanne na mke mmoja.
mwisho

No comments:

Post a Comment