Na Theonestina Juma, kyerwa
MWALIMU wa
shule ya msingi Mushisho Wilayani Kyerwa mkoani Kagera amejinyonga kwa kujitundika juu ya mti
na kuacha ujumbe uliosema kuwa amechukua hatua hiyo kutokana na msongo wa
mawazo yanayomkabili.
Kwa mujibu
wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa polisi
mkoani kagera, Phillip Kalangi tukio hilo limetokea Desemba 30, mwaka huu saa 4
asubuhi wilayani humo.
Mwalimu
aliyejinyonga kwa msongo wa mawazo amejulikana kwa jina la Medadi Rwabiga
ambapo jana hiyo alionekana akiwa amejitundika kwenye mti uliokuwa karibu na
nyumba yake.
habari zinadai kuwa wakati mwalimu huyo alichukua uamuzi wa kujitia kitangazi, mke na watoto wake walikuwa wameenda kanisani.
habari zinadai kuwa wakati mwalimu huyo alichukua uamuzi wa kujitia kitangazi, mke na watoto wake walikuwa wameenda kanisani.
Imeelezwa
kuwa tukio kama hilo la mwalimu huyo kutaka kujiua kwa kujinyonga si mara ya
kwanza, kwani mapema mwezi Desemba mwaka jana alifanya jaribio la kutaka kujiua
kwa kunywa dawa ya kuoshea mifugo.
Hata hivyo
katika jaribio hilo mwalimu Rwabiga hakufanikiwa kujiua kwani aliwahishwa
hospitalini na kupewa dawa na kuondoa sumu aliokuwa amekunywa kwa muda huo.
Hata hivyo
katika kuonesha kuwa bado alikuwa na dhamira hiyo ya kutaka kujiua ilitimia
hapo jana alipoamua kuchukua kamba na kutundika juu na mti na kujinyonga.
Habari zaidi
zinasema kuwa mwili wa mwalimu huyo ulichelewa kuondolewa katika eneo la tukio,
kutokana na tatizo la daktari kupatikana
mara moja.
Hata
hivyo kwa upande wa Kamanda Kalangi
alisema hadi sasa hawajajua chanzo kilichomfanya mwalimu huyo kuchukua jukumu
hilo nzito la kujinyonga na kwamba bado uchunguzi unaendelea.
“Jana
kulikuwa na tatizo la daktari na hivyo leo Desemba 31, mwaka huu ndiyo daktari
amepatikana na tayari polisi wako katika eneo la tukio kuufanyia uchunguzi
mwili wa daktari”alisem na kwamba mwalimu Rwabiga ameacha watoto wanne na mke
mmoja.
mwisho